Nipeni tena Kalamu, Nisome

Kijiji chetu Kandokando.
Nyumba na shule ni Mwendo.
Njiani kusonga na Mwendo.
Nipeni tena kalamu, Nisome.
Juma,Ali kuweka ndoano.
Ulaghai si wa Mfano.
Ndoto zangu  mkingamo.
Nipeni tena kalamu, Nisome
Magufuli naye kanena.
Elimu yangu si kitu tena.
Naweza kusonga tena.
Nipeni tena Kalamu, Nisome.
Nataka niwe rubani.
Kurusha ndege angani.
Ndoto zi bado hewani.
Nipeni tena kalamu,Nisome
Mimba yangu si ugonjwa.
Akili bado sijapunjwa.
Na ulimwengu nishafunzwa.
Nipeni tena kalamu, Nisome
Nipeni Tena Kalamu,Nisome

Na Alfred Kiwuyo,

Alfred ni mdau wa masuala ya vijana na watoto wa kike anayepatikana kwenye barua pepe alfredkiwuyo@gmail.com.  

One Comment

 1. Fadhy Mtanga says:

  Kuanguka si kushindwa,
  Hutokea nikatendwa,
  Haisaid’i kupondwa,
  Nipe kalamu nisome.

  Ninao wangu mchango,
  Sijafikia ukingo,
  Ndoto yangu ingalingo,
  Nipe kalamu nisome.

  Fadhy Mtanga,
  Mbeya, Tanzania.
  Jumanne, Julai 18, 2017.

Leave a Comment