Karibuni tena!

wewriteAsante kwa kufungua tena wavuti huu pendwa, tunatambua imekuwa muda sasa bila kusikia ama kuona makala nzuri za waandishi wachanga na wakongwe kutoka kwetu.

Hakika wasimamizi, waandishi na wadau mbalimbali wa wavuti hii walikuwa na hamu kuu ya kurudi tena hewani. Ni dhahiri wavuti huu umekua sehemu kuu katika kutoa fursa kwa wananchi wa kila ngazi na kundi kutoa mawazo na maoni yao kupitia maandishi. Hili ni jukumu na nafasi kuu inayotupa nguvu na hamasa ya kuona kuwa tunarudi na tunaendelea kuwepo na kukua kila uchao.

Niwahakikishie kuwa kwa sasa tumerudi rasmi na tunawakaribisha nyote kujumuika nasi, kusoma, kuandika na kubwa zaidi kutoa maoni kuhusu Makala mablimbali zitakazochapwa katika wavuti huu.

Uongozi wa WeWrite unaamini kuwa, mabadiliko na maendeleo yeyote katika nchi hupatikana hasa panapokua na jamii yenye fikra chanya, tunduizi, yenye kujadili na kung’amua mambo ndipo kufikia maamuzi na suluhisho lililo sahihi.

Kwa wenye kutaka kutuma kazi mbalimbali za uandishi iwe makala, mashairi nk watume kutumia baruapepe: submit@wewrite.or.tz

KARIBU TUENDELEZE GURUDUMU LA MAENDELEO.

KARIBU TUIJENGE TANZANIA.

Leave a Comment