Njia Mbadala ya Kupata Kazi Kiurahisi kwa Wasomi!

Na Hassan Pukey

 

Usomi wako unakusaidiaje?
Changamoto za Ukosefu wa Ajira nchini zimekithiri kiasi kwamba wasomi wamekuwa wakitoa lawama kwa Serikali hata kwa vitu vilivyo katika uwezo wao. Tunakaa na kulalamika kuhusu mitaala ya kufundishia sio rafiki, pengine sio rafiki ila nini maana ya usomi wetu tunapopata nafasi za kufanya maamuzi? Waziri, Mbunge, Afisa Elimu Mkoa, Tarafa, Wilaya wote walipitia katika mfumo wa Elimu huu uliopo.
Je, hawakuyaona haya? Na kama waliyaona wamechukua ama wanachukua jitihada gani kuweka mambo msawazo? Tusidanganyane ukweli ni kwamba wao ni wale miongoni mwa wale 7000 waliohitimu UDSM, UDOM na sehemu zingine. Kipindi walipokuwa shule walizungumza kuhusu hili la mitaala sio rafiki, wala haimjengi mwanafunzi kujiajiri. Je, leo wao wana nafasi ya kufanya marekebisho wanafanya hivyo?
Ushindani wa wasomi milioni 1.2 kila mwaka!
graduates-4

 

Lakini lengo langu si kumnyooshea mtu kidole, lengo langu hapa kumfungua mtu masikio aweze kusikia nilichokusudia kukisema. Kwa mwaka zaidi ya watu milioni 1.2 wanahitimu katika vyuo mbalimbali vya Ufundi Stadi na Vyuo Vikuu. Wachache kati ya hao wanafanikiwa kupata ajira, na kuacha kundi kubwa likikosa nafasi hizo. Asilimia 5% pekee ya milioni 1.2 ndio wanaopata ajira, kwa mujibu wa Shirika la Kazi (ILO) na Human and Economic Development Survey Report ya mwaka 2014/15. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Ukosefu wa Ajira umekuwa ukizidi kukua siku baada ya siku. Kama Elimu ya Ujasiriamali ikifundishwa kuanzia chekechea mpaka chuo itasaidia kwa kiasi? Au kama tukijenga vyuo kila mtu afike chuo Kikuu na kupata digrii itasaidia kwa kiwango gani kutatua tatizo la ajira kama chanzo ujinga uliokithiri.

 

Tabia yako inakukosesha ajira!
Unafahamu kuwa tabia ya mtu inachangia kwa kiasi cha asilimia 50 kukosa ajira? Kama unatabia mojawapo kati ya hizo ama zinazofanana jua ni moja ya vikwazo katika kupata ajira. Kijana unalala mpaka saa 4 Asubuhi na ukiamka ni kuangalia tamthilia ama kusikiliza muziki. Wengine wanadamkia Istagram kama afanyavyo Diamond ama Wema Sepetu, fahamu kuwa hawa wenzako kipato chao kinategemea asilimia 75 picha zao hata akiweka mswaki kwa wall yake maelfu kwa mamia watamuongelea tu na kumuweka Kwenye chati. Wewe unadamka na kuweka utupu au sura yako ambayo inaweza kugharimu katika kupata ajira.
Acha shuka saa 10 alfajiri!
Kuwa na kawaida ya kuachia shuka saa 10 Alfajiri kama mwanafunzi pata muda wa kupitia hata masomo yako. Kama kijana unayesubiri kazi za kuitwa na bahasha ya kaki kama mimi pitia hata vitabu vya Ujasiriamali ama vile vya Chakula cha Ubongo (Think Big, Creative, Critical). Hakikisha inapofika saa moja haurudi tena kitandani. Nenda hata ofisi za Serikali ya Mtaa ama Kata omba kusaidia kazi zilizo Kwenye uwezo wako pasi na malipo. Ukifanya ndani ya mwezi kuna kitu kimeongezeka, safari moja huanzisha nyingine.
Hassan Pukey ni kijana mwanaharakati anayejitolea na shirika la FEMA(FEMINA). Anapatikana kwa namba 0758279386 au barua pepe: hpukey@rocketmail.com

Leave a Comment