KONA YA USHAIRI: “DAKTARI”

Tulia

 

 

 

 

 

 

 

Daktari!
Daktari ameTulia hajaTulia?
Wajameni, lipi jibu sawia?
Akili kede si shaka amejaaliwa
Mihemko tele hakika amejaliwa…
Mwa vijana Dkt ametwaliwa
Kuhakikisha hoja zetu kubaniwa…
Mbobezi wa masuala ya sheria
Mchochezi wa tafrani na kadhia…
Mafunzoni, Magogoni, akaambiwa
Katu hoja pinzani kusikiwa…
Dkt ni mengi alidhaniwa
Miongoni mwao, wale wale, mesifiwa…
Dkt mwingi wa busara
Ilihali matendoye jawa papara…
Daktari…

 

AmeTulia, HajaTulia?

Tafadhali naomba kujibiwa.

Mtunzi wa shairi hili ni Jasper Kido ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii. Anapatikana kwa baruapepe; kidojasper@gmail.com na simu namba 0712 56 86 99

Leave a Comment