Masuala ya msingi anayopaswa kufahamu mpigakura siku ya kupiga kura

Nyerere katika mstari wa kupiga kuraSheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ndio sheria kuu inayohusu masuala ya uchaguzi nchini Tanzania. Sheria ya Uchaguzi pamoja na mambo mengine, ndio sheria inayoorodhesha na kutoa mwongozo yakinifu kuhusu namna chaguzi za wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinavyotakiwa kufanyika.

Sheria ya Uchaguzi imeoroshesha miongozo kuanzia namna ya kupendekeza wagombea wa nafasi za ubunge na nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, namna na muongozo wa namna ya kuchagua wagombea wa nafasi hizo ndani ya vyama vya siasa na namna Uchaguzi mkuu wa viongozi hao utakavyofanyika.

Sheria ya Uchaguzi pia, imeorodhesha vifungu vinavyotoa adhabu kwa mtu yeyote anaenenda kinyume na miongozo ya Uchaguzi.

Muongozo huu mfupi unadhamiria kumuelekeza mpiga kura kuhusiana na HAKI NA WAJIBU WAKE SIKU YA KUPIGA KURA, MAKOSA ANAYOTAKIWA KUEPUKA NAYO NA KUFAHAMU WATU PEKEE WANAORUHUSIWA KUINGIA KATIKA CHUMBA CA KUPIGIA KURA, kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Uchaguzi.

WAJIBU NA HAKI ZA MPIGA KURA

TAREHE 25 MWEZI OCTOBA 2015

Kituo cha kupiga kura

(a)  Kila mpiga kura ataweza kupiga kura pale atakapomkabidhi msimamizi wa kituo kadi ya mpiga kura au hati yoyote ile ya kupigia kura iliyoidhinishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

(b)  Baada ya kuona kadi ya mpiga kura, msimamizi wa uchaguzi atathibitisha uwepo wa jina la mpiga kura kwenye daftari la wapiga kura.

(c)  Baada ya hapo, Jina la mpiga kura litaitwa kwa sauti kubwa na msimamizi wa uchaguzi, ili maafisa waliopo katika chumba cha mpiga kura wasikie jina hilo likitajwa.

(d)  Msimaizi wa uchaguzi atampatia mpiga kura karatasi tatu za kupiga kura.

(e)  Karatasi hizi, moja ni ya wagombea wa nafasi ya urais, moja ni ya wagombea wa nafasi ya ubunge na moja ni ya wagombea wa nafasi ya udiwani.

(f)   Hakikisha karatasi yako ya kupigia kura ina muhuri maalum wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. KARATASI ISIYOKUWA NA MUHURI NI BATILI NA HAITAHESABIWA.

(g)  Ukishapata karatasi ya kupigia kura, mpiga kura ataenda katika sehemu maalaum ya kupigia kura, na kwa siri atarekodi kwa kuweka alama v katika kiboksi cha mgombea wa chaguo lake.

(h)Baada ya hapo, mpiga kura ataikunja karatasi yake ili kuficha kura yake na kisha kwenda kuitumbukiza karatasi ya kura katika boksi la kuwekea kura zilizokwisha pigwa.

Zingatia: mpiga kura hatakiwi kuonesha karatasi yake ya kura wakati umekwisha piga kura.Kura yako ni ya siri.  Kufanya hivyo ni makosa kisheria na kura yako itakua imeharibika.

(i)   Endapo mpiga kura hana uwezo wa kusoma, anaweza kusaidiwa kusoma na mtu yeyote wa chaguo lake isipokuwa wasimamizi wa kituo cha kupigia kura na mawakala wa vyama.

MAKOSA YA UCHAGUZI YANAYOMUHUSU MPIGA KURA KAMA YALIVYOAINISHWA KATIKA

SHERIA YA UCHAGUZI, 2010

  (i) Kuharibu muhuri wa tume katika karatasi ya kupigia kura.

(ii) Pasi kuwa msimamizi wa uchaguzi, kugawa karatasI za kupigia kura.

(iii) Kuweka katika boksi la kukusanyia kura zilizokwisha kupigwa, karatasi nyingine isiyokuwa karatasi maalum ya kupigia kura uliyopewa.

(iv) Kuchukua karatasi ya kupigia kura na kutoka nayo nje ya chumba cha kupigia kura.

(v) Kuharibu boksi la kuwekea kura zilizokwisha pigwa.

(vi) Kwa kutumia nguvu ama vitisho, kuzuia wapiga kura weninge wasipige kura

(vii) Kutoa rushwa kwa msimamizi wa uchaguzi ili aweze kupendelea mgombea wa upande mmoja

(viii) Mpiga kura; tambua pia kwamba, msimamizi wa uchaguzi akikupatia karatasi ya kupigia kura isiyo na muhuri maalum wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi basi, msimamizi huyo anaenenda kinyume na Sheria.

FAHAMU WATU PEKEE WANAORUHUSIWA KUINGIA KATIKA CHUMBA CHA KUPIGIA KURA

(i)  Msimamizi wa kituo

(ii) Msaidizi wa msimamizi wa kituo

(iii) Wakala wa Vyama

(iv) Mpiga kura

(v)  Mratibu Uchaguzi wa Mkoa

(vi) Mkurugenzi wa Uchaguzi

(vii) Mtu anaemsaidia mlemavu

(viii) Afisa na mwanachama  wa Tume ya Uchaguzi

(ix) Waangalizi wa uchaguzi walioruhusiwa

(x) Polisi

(xi) Afisa msimamizi wa  kura wa wilaya na msaidizi wake (Returning and Assistant Returning Officers)

Na Judith Salvio Kapinga

Judith ni mwanasheria anayepatikana Dar es Salaam

5 Comments

 1. Esther says:

  I love this, natamani nikisanye watu kule jimboni kwangu niwafundishe na wao pia ili tusipoteze kura
  Bravoooo

 2. philipo says:

  Hongera sana Judith kwa kutoa Elimu hii hata Mimi nimeweza kujua nayotakiwa kufanya kupitia makala hii

 3. hafidh says:

  elimu ya mpiga kura ni kitu muhimu sana kwani bila elimu kura zinaweza kuharibika

 4. Bellemeenah says:

  Oh Judy you never seize to amaze me! I love this,nimejifunza mengi sana

 5. John Kirigiti says:

  Very insightful and enlighting mydr!! Keep up the good work! Salute

Leave a Comment