Zaidi ya asilimia 50% ya wapiga kura wako katika mikoa 10

tanzania_political_mapMapema mwezi huu, ofisi ya Taifa ya Takwimu ilitoa makadirio ya idadi ya watu wanaotarajiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015. Idadi ya wapiga kura wa mwaka huu inakadiriwa kuwa watafika million 24.2 nchi nzima. Taarifa hiyo ilikuwa ikitoa  makadirio ya idadi ya watu wanaostahili kupiga kura katika majimbo ya uchaguzi Tanzania kwa mwaka 2015. Itakumbukwa kwamba, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, idadi ya wapigakura waliojiandikisha ilikuwa 20,137,303. Hata hivyo, watu walioshikiri kupiga kura katika mwaka 2010 walisemeana kuwa 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha.

Makadirio ya idadi ya wapiga kura katika mikoa mbalimbali yanatokana na uchambuzi wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Kwa mujibu wa sensa, Tanzania itakuwa na watu wapatao 48,522,229 ambapo watakaokuwa na umri wa kupiga kura watakuwa ni watu 24,252,927 endapo watu wote wanastahili watakuwa walipata fursa ya kujiandikisha kupiga kura. Hata hivyo pamoja na kwamba taarifa iliyotolewa na tume taarifa iliyotolewa na tume July 17, 2015 ikionyesha kukamilika kwa zoezi katika mikoa 17, inaonyesha uwiano wa moja kwa moja na takwimu za makadirio zilizotolewa na ofisi ya taifa ya Takwimu, taarifa ya tume inaonyesha kufika makaridio ya ofisi ya takwimu kwa zaidi ya asilimia 100.

Mwanzo wakati watangaza nia wa nafasi ya urais wakitafuta mwadhamini kabla ya kupitishwa na vyama vyao na hata baada ya vyama kupitisha wagombea rasmi, kuna mikoa ambyo haikuachwa kutembelewa. Hata sasa wakati vyama vikipita kuwatambulisha wagombea urais wake haswa cha chama tawala na UKAWA, kuna mikoa ambayo imekuwa ni target muda towe. Suala hili lilinifanya ni jaribu kufanya ufuatiliaji na uchambuzi mdogo wa kitamwimu kuelekea otoba 25.

Wazungu husema politics is a game of numbers, yaani ushindi wa kisiasa ni mchezo wa takwimu. Hii ina maana kwamba mwanasiasa haswa katika nafasi ya urais lazima atambue mahali ama makundi ya kijamii yenye watu wengi zaidi na ajikite katika mikakati ya kuwafika wapiga kura hao. Ni muhimu ikafahamika kwamba kuna maeneo yenye waiga kura wengi zaifi lakini yanaweza kuwa ma majimbo machache zaidi. Haya huwa ni maeneo ya kimkakati kwa kura ya urais.

Ikiwa watu million ishirini na nne nukta 3 (24,252,927) watakuwa wamejiandikisha na watapatiwa fursa ya kupiga kura basi zaidi ya nusu ya watu hao ambao ni kumi na tatu nukta 5 (13,520,000). Mkoa wa Dar es Salaam wenye majimbo nane utaongoza ukiwa na wapiga kura million 3 ukifuatiwa na Mbeya itakayokuwa na wapiga kura milioni 1.5. Mkoa wa Mwanza utakuwa na tatu ukiwa na wapiga kura milioni 1.4 na Morogoro itakayokuwa mkoa wa nne kwa wapiga kuwa wengi ambao ni sawa na milioni 1.3.Mkoa wa Kagera utakuwa katika nafasi ya 5 ukiwa na wapiga kura milioni 1.2 ukifuatiwa na Mkoa Tabora ambao unakadiriwa idadi ya wapiga kura milioni 1.1. katika orodha hiyo pia kutakuwa na Mkoa wa Tanga ambao una idadi sawa na mkoa wa tabora (milioni 1.1) na pia Dodoma katika nafasi ya nane ikiwa na wastani wa wapigakura milioni moja. Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ikiwa na wapiga kura laki tisa na elfu sabini sita (976,000) na laki tisa elf arobaini na nne (944,000) ndio inakamilisha mikoa yenye kumi bora za wapig kura.

Ukiachilia mbali mikoa hiyo kama kama nilivyoainisha hapo awali, mikoa mingine ambayo inatarajiwa na kichocheo kikubwa katika ushindi wa kura za urais ni pamoja na Mara (834,000), Geita (808,000), Ruvuma (783,000), Mtwara (773,000), Shinyanga (762,000), Manyara (741,000), na Simiyu (714,000). Mikoa inayotarajiwa kuwa na wapiga kura wachache zaidi ni pamoja na Mkoa mpya wa Katavi (271,000), Mkoa wa Mjini (347,000), Kaskazini Unguja (104,000), Kaskazini Pemba (103,000), Kusini Pemba (95,000) na Kusini Unguja (69,000).

Nadhani sasa watu wanaweza kuelewa kwanini ziara za wagombea urais zimekuwa zikilenga mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Zanzibar. Upande wa Zanzibar pamoja na kwamba mikoa yake inawapiga kura wachachewachache lakini Zanzibra yote kwa ujumla kama upande mmoja wa muungano una ushawishi mkubwa katika kukubalika kwa mgombea na kupelekea ushindi. Ni mbinu pia kwa mwanasiasa yoyote kuonyesha hitaji la kupata kuungwa mkono na wanzanzibar haswa ikizingatiwa kuwa kipindi ya zoezi la kutafuta katika mpya ya muungano ilijitokeza sana. Kukubalika kwa mgombea pande zote za muungano ni muhimu sana sio tu kwa kupelekea ushindi wa kuingia ikulu bali pamoja na uwezo wa mtu anayetaka kuwa rais kuweza kuitawala nchi pale atakapokuwa amefanikiwa kuingia madarakani.

Na Constantine Deus

Constantine ni mtafiti na mchambuzi

One Comment

  1. ATHANAS NYUNDO says:

    MAY GOD BLESS OUR GENERAL ELECTION

Leave a Comment