AYA MOJA: Vazi la Taifa li wapi?

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akipokea ripoti ya Kamati ya Vazi la Taifa

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akipokea ripoti ya Kamati ya Vazi la Taifa

Nchi ‘siyo tamaduni, basi imekufa,

Haijui ‘tavaa nini, basi ni ulofa,

Haijui vazi gani, liwe la taifa,

Tuelezeni, vazi la taifa li wapi?

Nchi yetu, kila kitu kina’we mchakato,

Nchi yetu, kila kitu kina’we mkato,

Nchi yetu, “kuwa tumeni jipatie pato”,

Tuelezeni, vazi la taifa li wapi?

Kwani Kiswahili, kilipatikanaje?

Sasa vazi hili, linakuwa gumuje?

Hiyo michoro dili, au mnaichunguzaje?

Tuelezeni, vazi la taifa li wapi?

Mliunda tume, kuzunguka nchi nzima,

Wake na waume, tena watu wazima,

Tovutiye ‘kumbwa ukame, haina kitu mwaka mzima,

Tuelezeni, vazi la taifa li wapi?

Bado siamini, kama twakosa vazi,

Lichukuliwe la umasaini, lililodumu vizazi,

Siasa kwenye utamaduni, inaharibu kazi,

Tuelezeni, vazi la taifa li wapi?

Na Naamala Samson

Samson ni Makamu Mwenyekiti wa shirika la TYVA.

Leave a Comment