AYA MOJA: Meli imekosa dira

Ship

“Nahodha ongeza mwendoooo” abiria wanashangilia,

Meli inapoenda hawapajui wasije wakalia,

Hii meli yetu nzuri kila mtu anaifagilia,

Ila ina matatizo kibao nitakusimulia,

Kwanza haijulikani inatumia dira gani,

Mara inaenda kusini mara kaskazini,

Inaenda kadri kinachomjia nahodha kichwani,

Kuna siku aliwahi kutusimamisha baharini,

Kwanini?akajibu kuwa ye mwenyewe hajui!.

Yani hajui kwanini tumesimama!

Yani hajui kwanini tumekwama!

Yani hajui kwanini meli imezima!

Tukakaa baharini siku nzima!

Wengine wakasema “tuijaze maji ya bahari”,

Wengine wakasema “tuongeze mawe ya shadari”,

Na wengine wakasema “tuyamwage mafuta kwenye bahari”,

Tukafanya vyote ila haikwenda tukabaki tunatafakari,

Abiria wengine wakachoka baharini wakajitupia,

Ndugu zangu wengine kwa njaa wakajifia,

Waliokuwa na silaha kali risasi wakajirushia,

Wapo waliomshambulia nahodha mawe kumrushia,

Meli tulizokuwa nazo sawa mbele zimeshasonga,

Na huko ziendako nanga zimeshatinga,

Sisi tumebaki nyumba mwamba tumegonga,

Twangoja dira aje kutupa mganga!!

Na Naamala Samson

Samson ni Makamu Mwenyekiti wa shirika la TYVA.

Leave a Comment