Je mchawi ni yupi Arsenal?

Arsene Wenger

Arsenal imepata kiasi kikubwa cha pesa baada ya kuwauza wachezaji wake Cesc Fabregas(Barcelona), Samir Nasri(Man City), Gael Clichy(Man City) na Eboue nilitegemea baada ya kupata kitita hiki wangetafuta wachezaji wenye uwezo mkubwa ili kuziba mapengo hayo. Cha kushangaza ni kuona wanasajili wachezaji ambao hawana uwezo wa kutosha kwa kukosa uzoefu.

Arsenal imewasajili wachezaji kama Gervinho(Lille), Park(Monaco), Chamberlain(Southampton), Garl Jenkison(Charlton).“Makinda” hawa hawawezi kupambana na mikikimiki ya kina Drogba, Rooney, Anelka, Dzeko, Aguero na wengine,hakuna ubaya kusajili makinda lakini ni bora pia uangalie na hitaji husika kwa wakati tofauti na hapo ni kupelekea kuanza upya kwa timu na matokeo yake ni kuanza vibaya kwa Arsenal msimu huu na kikubwa zaidi ni kipigo cha udhalilishaji walicho kipata kutoka kwa Manchester United kwa kufungwa magoli 8-2.

Sir Alex Ferguason amenunua wachezaji makinda lakini ameangalia uzoefu, Phil Jones kutoka Blacknurn Rovers ambaye alicheza msimu mzima akiwa na timu yake hiyo, pia uzoefu wa walioupata wachezaji wake Dany Welbeck(Sunderland), Tom Cleverley(Wigan) na Diouf(Blackburn) pia wamepata uzoefu wa kutosha hili linajithibisha kwa kuona kiwango kikubwa alichokionyesha Tom Clevery na Welbeck tangu msimu huu ulipoanza.Mechi kati ya Manchester United imethibitisha kuwa vijana wa Arsene Wenger hawajakuwa na uwezo wakupambana na timu kubwa pale uingereza, vijana hao walizidiwa kila pande na Manchester United.

Kitendo cha kukosa ubingwa wa ligi kuu kwa takribani misimu sita na mabadiliko haya yaliyotokea sitegemei jipya kutoka kwao na kitu ninachodhani hata nafasi nne bora hawatakuwepo hii ni kutokana na kuwepo timu zilizojiandaa na kufanya usajili mzuri,timu kama Manchester City, Chelsea, Liverpool na Manchester United.

Mabadiliko yalazima yanatakiwa yafanyike ili kuifanya timu hii irudishe hadhi yake na imani kwa mashabiki wake kwani wale wenye mioyo ya wasiwasi iliyochoshwa na mfumo huu wamehamia Manchester City kwa mkopo.

Na Ally Shambi

Mchambuzi wa masuala ya michezo.

 

Leave a Comment